London, England. Mkongwe wa Arsenal, Ian Wright amedai kuwa Arsene
Wenger amemwambia kuwa anakaribia kuachana na kazi ya kuifundisha timu hiyo.
Mkataba wa Wenger mwishoni mwa msimu huu na bado
hajasaini mkataba mpya na alikataa kuzungumzia maisha yake ya baadaye klabuni
hapo.
Wright alikutana na Wenger juzi na alionekana
kuchoka, akibainisha kwamba Mfaransa huyo ameonyesha kila dalili kuwa ataachia
ngazi baada ya kuinoa miamba hiyo kwa miaka 21.
Akizungumza na BBC Radio 5Live Ijumaa usiku,
Wright alisema: “Nilikuwa na kocha (Wenger) jana usiku na kama natakiwa kusema
ukweli, nimeona dalili kwamba nadhani natakiwa kumwamini alichoniambia.
“Nilikuwa nae kwa saa chache usiku, tulizungumza
na kiukweli hakuniambia moja kwa moja kama ‘naondoka mwishoni mwa msimu’.
Nimeona dalili tu, kwamba kama aliyechoka hivi.
“Alichoniambia moja kwa moja ni kwamba anaelekea
ukingoni mwa kazi yake. Sikjawahi kumsikia akisema hivyo kabla.”
Wenger na Wright walikuwa katika hafla ya Q&A
kwenye Uwanja wa Emirates Alhamisi usiku kabla ya mchezo wao wa jana wa ushindi
wa mabao 2-0 dhidi ya Hull City.
Kocha huyo wa Arsenal amekuwa katika presha ya
mashabiki wanaomtaka ajiuzulu kutokana na kufungwa mara mbili mfululizo dhidi
ya Watford na Chelsea, kitu kilichoathiri mipango yao ya ubingwa msimu huu.
Kushindwa kwa Wenger kutwaa taji la Ligi Kuu
England tangu 2004 kumewafanya mashabiki wamshambulie kwa maneno, huku wengine
wakibeba mabango yenye ujumbe wa kumtaka aachie ngazi, walipofungwa kwenye
Uwanja wa Stamford Bridge wiki iliyopita.
Akiwa na miaka 67 sasa, kocha huyo Mfaransa ndiye
mkubwa zaidi na kocha mwenye muda mrefu katika klabu moja kuliko wote wa Ligi
Kuu England.
Anaonekana amechoka,” aliongeza Wright, wakati
akiwa katika kipindi juzi alipoulizwa juu ya majaliwa ya Wenger.
0 comments:
Post a Comment