Dar es
Salaam. Licha ya kuandamwa na tuhuma za kughushi vyeti, Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hawezi kuzungumzia suala hilo kwani
majibu yake yapo mtandaoni sakata lilipoanzia.
Makonda
amesema hayo leo (Ijumaa) alipoulizwa swali na wanahabari kuhusu uhakika
wa taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa alinunua vyeti na kutumia jina lisilo
lake.
"Maswali
ya mitandaoni yanaishia mitandaoni siko hapa kupoteza focus (mwelekeo).Ukiona
maneno mengi yanaibuka kwenye ishu ya dawa za kulevya ndiyo ujue vita imefika
penyewe,"amesema Makonda.
0 comments:
Post a Comment