Wapinzani wengi wa
rais wa Marekani Donald Trump, wanaamini kuwa itawabidi wasubiri kwa miaka
minne ili aweze kuondoka madarakani.
Lakini wachawi nchini
Marekani hawakubaliani na hilo.
Usiku wa manane siku
ya Ijumaa, wale wanaoamini uchawi kote nchini Marekani, waliandaa matambiko
yenye nia ya kumuondoa Trump uongozini.
Hadi sasa ukurasa wa
Facebook wa matambiko huyo umepata wafuasi 10,500.
Hatua hizo zimezua
ghadhabu kotoka kwa wakirsto ambao wamewalaumu wachawi hao wa kutangaza vita
vya kiroho.
Wachawi hao wanapanga
kurudia tambuko hilo hadi pale Trump atakapoondoka ofisini. Tambiko lingine
litafanyika machi 26.
Chama cha wakiristo
nacho kilitangaza tarehe 24 mwezi Februari kama siku ya maombi ya kuukabili
uchawi huo.
Hata hivyo Trump
hajazungumzia lolote kuhusu vita hivyo kati ya kanisa na uchawi.
0 comments:
Post a Comment