Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania limeonya vikali na kupiga marufuku watu
kuingiza siasa katika mchezo wa leo kati ya Simba na Yanga
Akiongea leo na waandishi wa habari,Afisa
Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa wamepata taarifa kuna watu
fulani leo wanataka kuchana kadi za chama fulani, wengine wanataka
kuchoma bendera za chama fulani kupitia mchezo wa leo kati ya Simba na
Yanga, hivyo wameonya vikali watu wasijaribu kuingiza siasa zao kwenye
michezo na kusema kwa yoyote atakayejaribu yatakayompata asije kuwalaumu
TFF
"Kuna
watu tumesikia na kuthibitishiwa kwamba kuna watu leo wanataka kuchana
kadi za chama fulani cha siasa uwanja wa Taifa mbele ya mashabiki wa
Simba na Yanga.
"Kuna wengine wamepanga kuzichoma moto, wako wale wengine wamepanga kuchoma hata bendera za chama hicho, wengine wanasema watafanya ndani ya uwanja wengine nje ya uwanja.
"Nitumie nafasi hii kuwaambia kwamba taarifa tunazo na tunatoa onyo kali kwa yoyote atakaye thubuti kufanya hayo wanayotaka kufanya kwani litakalo mtokea lisijekuwa lawama kwa TFF" alisema Alfred Lucas.

0 comments:
Post a Comment