Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda,
ametangaza kuunda serikali sambamba na utawala uliopo Rwanda, lakini
itakayokuwa ikifanya kazi nje ya nchi.
Katika mazungumzo na BBC, mwanasiasa huyo anasema lengo la serikali yake ni kuiondoa madarakani serikali ya rais Paul Kagame, anayemlaumu kuvunja sheria na kukandamiza wananchi.
Thomas Nahimana, amekatazwa kuingia Rwanda kujiandikisha kama mgombea wa kiti cha urais, katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Baraza lake la mawaziri
Ametangaza tayari baraza lake la mawaziri.Baadhi ya aliowataja katika baraza lake la mawaziri ni wafungwa wanaotumukia vifungo vya jela nchini Rwanda kwa makosa kama vile kukanusha kuwa mauwaji ya kimbari hayakufanyika nchini Rwanda mwaka 1994.
Chama chake cha Ishema, bado hakijaandikishwa nchini Rwanda.








0 comments:
Post a Comment