By Hadija Jumanne, Mwananchi
Dar es Salaam. Wanafunzi wanne wa Chuo
Kikuu cha Kampala(KIU) kampasi ya Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama
ya Wilaya ya Ilala, kujibu shitaka la kusambaza picha za kumkashifu Rais John
Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp.
Washitakiwa hao ni Amenitha Kongo(19),
Maria Tweve (20), Agnes Gabriel(21) na Anne Mwansasu(21), ambapo wamepandishwa
mahakamani hapo leo na kusomewa shtaka linalomkabili mbele ya Hakimu
Mkazi Catherine Kiyoja.
Kwa pamoja washtakiwa hao
wanadaiwa kuchapisha picha ambazo zinaonyesha Rais Magufuli akiwa amevaa hijabu
kama mwanamke wa Kiislamu na kuzisambaza kwenye mtandao huo wa WhatsApp,
huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Washtakiwa wamerudishwa rumande baada
ya kushindwa kitimiza masharti ya dhamana.
0 comments:
Post a Comment