Rais Museveni pia atatembelea maeneo mengine muhimu katika ushirikiano kati ya Uganda na Tanzania. Maeneo hayo ni pamoja na kiwanda cha Bakhresa kilichopo Vingunguti na bandari ya Dar es Salaam.
Akizungumzia ziara hiyo ya kwanza ya Museveni nchini tangu Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani, Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Augustine Mahiga amesema viongozi hao watakuwa na mazungumzo yao, baadae watakuwa na mazungumzo ya pamoja na maofisa wa pande zote.
Dk Mahiga amesema katika mazungumzo yao, wataongelea hatua waliyofikia katika ujenzi wa bomba la mafuta linalotoka Hoima, Uganda mpaka Tanga, Tanzania.
Thursday, February 23, 2017
Rais Museveni kutua nchini Jumamosi
2:55 PM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment