Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape
Nnauye ametoa salamu za pole kwa Rais wa Shirikisho la Riadha
nchini, Anthony Mtaka kufuatia kifo cha mshiriki kutoka nchini Kenya, Charles
Rioba (36) aliyefariki katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon
yaliyofanyika Februari, 26 mkoani Kilimanjaro.
Rioba alishiriki kwa hiari mbio
zijulikanazo kama ‘run for fun’ za Kilometa 21, zilizohusisha wananchi
mbalimbali wakiwemo pia viongozi wastaafu.
Lakini akiwa katika mbio hizo alianguka
na kupatiwa huduma ya kwanza kisha kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) na baadae kufariki dunia.
Waziri Nape ametoa pole pia kwa
waandaaji wa mashindano hayo na wote ambao wameguswa na msiba huo
0 comments:
Post a Comment