By Azory Gwanda, Mwananchi
Kibiti. Watu
watatu akiwamo OCCID wa Wilaya ya Kibiti, Peter Kubezya wamefariki dunia kwa
kupigwa risasi na watu wadhaniwa kuwa ni majambazi katika Kijiji cha
Jaribu wilayani hapa.
Mkuu wa
Wilaya ya Kibiti, Gullamuhusein Kifu amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na
kusema watu sita wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za moto
walikivamia kituo change Wiley's cha kukusanyia ushuru kilichopo kijijini hapo.
Taarifa za
awali zimeeleza kuwa mauaji hayo yametokea usiku wa kuamkia leo Jumatano
ambapo watu hao wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa na bunduki walivamia
kuzuizi cha maliasili kilichopo kijijini hapo na kukichoma moto kabla ya
majibizano ya risasi na polisi wakiokuwa doria kwenye eneo hilo.
Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Misheni ya Mchukwi, Zakaria Lukeba amethibisha kufikishwa
kwa mwili Kubezya ukiwa na jeraha la risasi tumboni pamoja na maiti mbili
ambazo hazijajulikana majina.
0 comments:
Post a Comment