Social

Thursday, February 23, 2017

TCU yaibuka na mapya




By Kelvin Matandiko, Mwananchi kmatandiko@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Vumbi la kukosa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu likiwa halijatulia, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema zaidi ya wanafunzi 8,000 wa vyuo vikuu 52 nchini wapo njiapanda ya kuendelea na masomo baada ya uhakiki kukamilika.
Taarifa ya TCU iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, imeeleza kuwa imewabaini wanafunzi ambao wamedahiliwa katika programu ambazo hawana sifa.
Orodha ya wanafunzi hao tayari imewasilishwa kwenye vyuo vikuu vya Dar es Salaam (UDSM), Dodoma (Udom), Mtakatifu Augustine (Saut) na Tumaini.
Hata hivyo, hatua hiyo ya TCU imekosolewa na wadau wa elimu wakisema Tume hiyo ilifanya uzemb,e kwani ilikuwa na uwezo wa kutambua kila mwanafunzi asiyekuwa na sifa kwa kutumia mfumo wake wa udahili (Central Admission System).
Uhakiki huo unatokana na agizo Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alilotoa Agosti mwaka jan baada ya kutangaza kuwapo kwa wanafunzi ‘hewa’ na ‘vihiyo’ ambao wanapatiwa mikopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).


0 comments:

Post a Comment