Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mwenzake Revocatus Muyela wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya Aneth Msuya.
Hata hivyo muda mfupi baada ya kuachiwa huru, askari polisi wamewakamata tena na kuwapandisha kwenye gari polisi na kuondoka nao.
Awali, Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa aliwaachia huru washtakiwa hao baada ya upande wa mashtaka kushindwa kufanya marekebisho ya hati ya mashtaka ya mauaji ya kukusudia iliyokuwa ikiwakabili mahakamani hapo.
Hatua hiyo ilifikiwa baada ya jalada la kesi hiyo lililokuwa limeitwa Mahakama Kuu kurejeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Februari 20, 2017 Hakimu Mwambapa aliupa upande wa mashtaka muda wa siku tatu kurekebisha hati ya mashtaka.
0 comments:
Post a Comment