Dar es
Salaam. Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) limetoa siku
14 kwa Serikali kuwarejeshea wafanyakazi fedha za mikopo ya elimu ya juu
wanazokatwa kimakosa vinginevyo watafanya uamuzi mgumu
Akizungumza
leo (Jumanne) Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokwa amesema wafanyakazi hao
waliingia mkataba na Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ya
kukatwa asilimia nane.
Amesema
baada ya sheria mpya iliyopitishwa Agosti 2016 imebadilisha na sasa wanakatwa
asilimia 15 bila kujali walikopa lini mikopo hiyo.
"Tunataka
waliokopa kabla ya kupitishwa sheria hii waendelee kukatwa asilimia nane na
siyo asilimia 15 wanayokatwa" amesema.
0 comments:
Post a Comment