Tetemeko la ardhi ya
ukubwa wa 5.7 kwenye vipimo vya Richter limekumba maeneo ya Ziwa Tanganyika
usiku wa kuamkia leo.
Tetemeko hilo
lilitikisa maeneo ya kaskazini mwa Zambia na mitetemeko hiyo ikasikika maeneo
ya kusini magharibi mwa Tanzania, hasa eneo la Rukwa.
Kitovu cha tetemeko
hilo, kwa mujibu wa Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani, kilikuwa
kilomita 10 chini ya ardhi umbali wa kilomita 45 mashariki mwa mji wa Kaputa
nchini Zambia.
Mji huo unapatikana
katika mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Tetemeko hilo
lilitokea mwendo wa saa tisa na dakika thelathini na mbili usiku (0032 GMT).
Tetemeko la ardhi la
ukubwa kama huo huchukuliwa kuwa la kadiri lakini wataalamu wanasema kutokana
na hali kwamba kitovu chake chakikuwa chini sana ndani ya ardhi, huenda hilo
lilisababisha mitikisiko kuwa mikubwa.
Desemba mwaka 2005,
tetemeko kubwa la ardhi lilitokea eneo la Ziwa Tanganyika.
Tetemeko hilo la nguvu
ya 6.8 lilitikisa majumba katika miji maeneo ya Afrika mashariki na kati.
0 comments:
Post a Comment