By Hussein Issa, Mwananchi
hissa@mwananchi.co.tz
Dar es
Salaam. Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ( TCU)
imetoa
ufafanuzi kuhusu wanafunzi 8,357
waliotajwa kuwa hawana sifa stahiki za kuendelea na elimu
ya juu na kudai kwamba kulikuwa na dosari katika taarifa zao.
Taarifa
kutoka TCU kwa vyombo vya habari imesema kuwa uhakiki wa
sifa za wanafunzi ni kazi endelevu ya tume na kutokana na maombi ya wadau
mbalimbali ,tume sasa itaendelea kuwasiliana moja kwa moja na vyuo
katika kukamilisha zoezi hilo.
Taarifa
hiyo imesema wanafunzi wote walioorodhesha katika taarifa
iliyotolotewa awali wanaombwa kuwa watulivu na kuendelea na masomo
yao ya kawaida.
“TCU
inapenda kuuarifu umma kuwa ,uhakiki wa ubora wa
wanafunzi wa elimu ya juu hufanyika kwa mujibu wa kifungu 5(1)(b)c) cha Sheria
ya Vyuo vikuu Sura ya 346 YA Sheria za Tanzania,’’imesema taarifa hiyo.
0 comments:
Post a Comment