Social

Thursday, February 23, 2017

Makonda: Changamkieni fursa za biashara




Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wakazi wa jiji hilo kuchangamkia fursa za biashara wakati wa  ujio wa marais wa wawili wanaotarajiwa kuwasili nchini hivi karibuni.
Marais hao ni Yoweri Museveni wa Uganda na Danny Faure wa visiwa vya shelisheli.
Kwa mujibu wa Makonda ziara ya Museveni itaanza Februari 25 hadi 26 wakati ya Rais Faure itakuwa kati ya Februari 27 na 28.
“ Wageni hawa watakuja na misafara ndipo hapo suala la biashara linapokuja, tutumie fursa hii kufanya biashara na kutangaza vivutio tulivyonavyo,”amesema Makonda.

0 comments:

Post a Comment