Dar es
Salaam. Wanamuziki Ally Kiba na Diamond Platnumz ni miongoni wa wajumbe wa
kamati ya watu 10 wa kusaidia maandalizi ya timu ya taifa ya vijana ya
Tanzania 'Serengeti Boys'
Akitangaza
kamati hiyo inayoundwa na wanahabari, viongozi wa kampuni na wasanii Waziri wa
Habari, Utamaduni Sana'a na Michezo Nape Nnauye amesema jukumu kubwa la kamati
hiyo ni kuhakikisha wananchi wanashirikishwa kwenye maandalizi ya timu hiyo.
"Tumeshamiria
kuona timu hii inafanya maandalizi makubwa na nimeongea na Malinzi asubuhi hii
yuko Morocco akiweka sawa masuala ya kambi ya vijana,"amesema.
Kamati
hiyo itakuwa chini ya uenyekiti wa mwanahabari mkongwe Charles Hillary na
katibu ni katibu mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine.
Wajumbe wa
kamati hiyo ni wanamuziki Ally Kiba na Diamond Platnumz wengine ni Beatrice
Singano, Ruge Mutahaba, Maulid Kitenge, Erick Shigongo, Hassan Abbas na
mwanamitindo Hoyce Temu.
Serengeti
Boys imefuzu kucheza fainali za vijana Afrika nchini Gabon Mei 24- Juni 5,
baada ya kushinda rufani yake dhidi ya Congo-Brazzaville iliyomchezesha
mchezaji Langa Lesse Bercy ambaye umri wake ulizidi miaka 17.
0 comments:
Post a Comment