Aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya
Leicester Claudio Ranieri amesema kuwa ndoto yake imepotea wakati
alipopigwa kalamu kama kocha wa klabu hiyo miezi tisa baada ya kuisaidia
kushinda taji la ligi.
Leicester sasa iko pointi moja juu ya eneo la kushushwa daraja huku ikiwa imesalia mechi 13.
''Baada ya furaha ya mwaka uliopita na kushinda taji la ligi nilikuwa na ndoto ya kusalia na Leicester.Kwa bahati mbaya haikuwezekana''.
''Fursa hiyo ilikuwa nzuri na itakuwa nami maishani''.
''Ninamshukuru kila mtu katika klabu hiyo,kila mtu aliyeshiriki katika ufanisi ,hususan mashabiki''.
''Muliniweka katika nafsi zenu kuanzia siku ya kwanza na kunipenda.Ninawapenda nyie pia nami''.
''Hakuna mtu anayeweza kuchukua kile tulichofanikiwa kupata pamoja na natumai munalifikiria hilo na kutabasamu kila siku ninavyotabasamu''.
0 comments:
Post a Comment