Dar es
Salaam.Moto uliowashwa na Serikali, kuzuia kuuzwa kwa pombe kali
zinazowekwa kwenye mifuko midogo ya plastiki, maarufu viroba umetapakaa barani
Afrika.
Wakati
zikiwa zimesalia siku tano kabla ya kuanza kutekelezwa kwa amri hiyo, nchini
Malawi sakata hilo limekuwa ni vita kati ya “afya na biashara”.
“Pombe ina
madhara hasi katika ubora wa mfumo wa elimu,” alisema Mkuu wa
Sekondari ya Livuzu ya Blantyre, P. Simbota alipozungumza na gazeti
la Nyasa Times.
“Pakiti
hizi zina kiwango kikubwa cha kilevi na zinauzwa kwa bei ndogo. Wanafunzi
hunyonya wakati wa masomo, kwa kuwa ni ndogo na rahisi kuzificha. Wengine
huchanganya hata na maji ya kawaida au juisi na hivyo kuficha tabia zao
hatarishi.”
Tayari,
Serikali nchini imepiga marufuku pombe hizo, ambazo nyingi huwa na kiwango cha
kilevi kinachofikia kati ya asilimia 30 na 40, kwa maelezo kuwa zinachafua
mazingira, ni rahisi kutumiwa na vijana wadogo na hata watoto wa shule za
msingi.
0 comments:
Post a Comment