BAADHI ya mawaziri waandamizi wanaripotiwa kutaka kuhamisha misaada kutoka katika miradi ‘inayopoteza’fedha barani Afrika na Asia kwenda kwa washirika wa Uingereza huko Ulaya mashariki ili kufaidika na makubaliano ya Brexit.
Maafisa katika ofisi ya Waziri Mkuu huko Downing Street na mawaziri waandamizi wanaamini kuwa sehemu ya bajeti ya serikali ya paundi bilioni 12 kwa ajili ya misaada inapaswa kutumiwa kwa ajili ya kupata uungwaji mkono ili kupata makubaliano mazuri na Brussels, makao makuu ya Umoja wa Ulaya.
Kulingana na gazeti la The Sunday Times, pendekezo hilo litashuhudia fedha za misaada zikiondolewa kwenye miradi ‘isiyoeleweka’ katika nchi zinazoendelea huko Asia na Afrika na kupelekwa huko Poland, Hungary na nchi za Baltiki, ambazo hadi sasa ni washirika wa Uingereza.
Hatua hiyo inaripotiwa kuwa inalengo la kuzishawishi nchi za Ulaya mashariki kuiunga mkono nchi hiyo, wakati ikiwa katika mazungumzo ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya.
Lakini mapendekezo hayo yaliyojaa utata yameshaanza kusababisha vita baina ya mawaziri na maafisa katika Wizaya ya Maendeleo ya Kimataifa, DfId, gazeti hilo linasema.
DfId inasisitiza kwamba mpango huo unakwenda kinyume na batili kulingana na sheria za kimataifa kwa kuwa nchi pekee ambazo zinafuzu kwa ajili ya fedha za maendeleo katika Ulaya mashariki ni Ukraine na Albania, ambazo sio wanachama wa Umoja wa Ulaya.
Sheria juu ya nchi ambazo zinastahili kupewa misaada ya maendeleo zinaandaliwa na Organisation for Economic Co-operation and Development (OECD).
Chanzo kimoja cha juu serikalini kililiambia gazeti la The Sunday Times kwamba mawaziri wamekuwa wakitazama fedha za misaada kwa “macho ya njaa.”
Maafisa wengine wa ngazi za juu walisema kwamba Waziri wa Mambo ya Nje Boris Johnson, Waziri wa Ulinzi Sir Michael Fallon na mawaziri wengine walitaka kuona bajeti hiyo ikielekezwa katika jitihada za kuboresha makubaliano ya Brexit. Chansela Philip Hammond pia anaripotiwa kuwa anapendelea wazo hilo.
Hili linakuja baada ya Johnson kutangaza kwamba atatenga hadi paundi milioni 7000 kutoka kwenye bajeti ya misaada ili kuboresha nguvu za Ukraine na mataifa ya Baltiki, ambazo zinakabiliwa na kuongezeka kwa uchokozi wa Urusi.
Mbunge wa chama cha Labour Mike Gapes, ambaye ni mwanachama wa Kamati ya Masuala ya Kimataifa, aliliambia gazeti la The Independent kwamba taarifa hiyo imevjishwa wiki chache zilizopita kabla bajeti mpya kutangazwa na kwamba kwa sasa ni suala la kusubiri na kuona inakuaje.
0 comments:
Post a Comment