Social

Friday, February 24, 2017

Mbowe, Wema damudamu



Dar es Salaam. Hii ni baada ya mrembo wa Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu kujitokeza mahakamani kumsindikiza Mwenyekiti wa  Chadema, Freeman Mbowe katika kesi ambayo mbunge huyo wa Hai amefungua dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, Simon Siro na sasa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Jana, Wema alikuwa Mahakama Kuu akionekana mwenye furaha na wakati fulani akinyoosha vidole viwili, alama inayotumiwa na Chadema. Alikuwa amekaa karibu na Mbowe, huku pembeni akionekana Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya.
 Wakati Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alipojitokeza juzi kumtetea msanii huyo, ilionekana ni jukumu lake la kawaida la kiwakili lakini jana ndipo ilipodhihiri siri iliyokuwa ndani.

Picha za Wema zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na muda mfupi baadaye ofisa habari wa Chadema, Tumaini Makene alituma ujumbe ulioarifu kuwa Mbowe angeongea na umma kupitia vyombo vya habari.

0 comments:

Post a Comment