Dar es
Salaam. Ikiwa imetimia miaka miwili tangu kifo cha aliyekuwa kada maarufu wa
Chama cha Mapinduzi CCM, Kapteni John Komba, Mke wake Salome Komba
ameibuka na kumuomba mwenyekiti wa Chama hicho Rais Dk John Magufuli amsaidie
ili aweze kulipwa 'Mafao' na 'Stahiki' za mume wake.
Akiongea
kupitia kipindi cha Maisha Mseto cha Times Fm mapema leo (Jumanne)
asubuhi, Salome amedai kuwa wanaidai CCM mafao ya Sh75 milioni kama
jasho la mume wake alivyokitumikia CCM lakini hadi sasa wamelipwa Sh4.5
milioni.
"Namuomba
Mwenyekiti wa CCM anisaidie niweze kupata mafao ya marehemu, alikuwa anaipenda
sana CCM na mpaka anafariki alikuwa ameanza kuwahamasisha wasanii kuhusiana na
kampeni," amesema na kuongeza:
"Niliongea
na Katibu Mkuu, nikamweleza nadai Sh75 milioni ila nimepewa Sh4.5 milioni na ni
mwaka wa pili sasa hivi tangu mume wangu afariki, hivyo naomba nisaidiwe nipate
jasho lake kwa sababu ni haki yake kwa jinsi alivyojitoa kwenye chama, na
amefariki akiwa ndani ya CCM."
0 comments:
Post a Comment