Zanzibar.
Siku chache baada ya Jeshi la Polisi Zanzibar kutoa orodha ya majina 42 ya
watuhumiwa wa dawa za kulevya, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Ayoub
Mohamed Mahmoud ametoa majina 14 ya askari wanaotuhumiwa kushirikiana na
waingizaji na wauzaji wa dawa hizo.
Mahmoud
alitoa taarifa hiyo jana alipozungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa
Sanaa uliopo Rahaleo mjini hapa. “Bado tunaendelea kuwasaka watu wengine na
tumeongeza ulinzi katika maeneo mengi,” alisema Mahmoud.
Alisema
watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa, wakati wowote watafikishwa mahakamani kujibu
tuhuma zao.
Mkuu huyo
wa mkoa alisema hawawezi kutaja majina ya askari hao hadi pale uchunguzi
utakapokamilika.
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya dawa za kulevya, Rogers Sianga alisema atahakikisha hakuna
mtu hata mmoja anayeingiza, kuuza au kutumia dawa za kulevya nchini.
“Mipango
maalumu imeandaliwa ili kudhibiti hali hiyo na kuhakikisha kuwa maeneo yote
yaliyokuwa yanatumiwa na kundi hilo la uingizaji na uagizaji wa dawa za kulevya
yanadhibitiwa,” alisema.
Alisema
kuna wajanja wanaovitumia visiwa vya Zanzibar kama kimbilio la kujificha.
Kamishna
huyo alisema kuanzia sasa nguvu zaidi zitaelekezwa visiwani humo katika maeneo
ya viwanja vya ndege na bandari ili kuhakikisha hakuna dawa itakayoingia.
Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali
alisema wanafanya mchakato wa kuongeza mashine maalumu ya kufanyia uchunguzi
katika maeneo ya viwanja vya ndege, bandarini na maeneo yanayopokea mizigo
kutoka nje.
0 comments:
Post a Comment