Social

Wednesday, March 29, 2017

Ndesamburo ataka Tanga iwe ngome ya Chadema


Tanga. Mgombea uenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Philemon Ndesamburo amesema Tanga inahitaji nguvu zake za ziada kuhakikisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vinashinda kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Amesema hayo jana baada ya  kuwasili kwenye Hoteli ya Mkonge jijini hapa kinapofanyika kikao  cha Kamati Kuu.
Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuingia kwenye kikao hicho, Ndesamburo amesema: "Kati ya mikoa minne ya kanda hii ya Kaskazini, Tanga bado inatutia unyonge sisi Ukawa, hapa ni ngome ya CCM. Nikichaguliwa nitakuja kuweka ngome hapa."
Kikao cha Kamati Kuu kilianza jana saa 9:45 alasiri baada ya kuwasili Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na wajumbe wa mkutano huo.

0 comments:

Post a Comment