Social

Tuesday, March 28, 2017

Jeshi la Kenya lawaua wanamgambo 31 wa al-Shabab


Jeshi la Kenya lawaua wanamgambo 31 wa al-shabab

Wanajeshi wa Kenya wameripotiwa kuwaua wanamgambo 31 wa al-Shabab, baada ya kushambulia kambi yao eneo la Badhade kusini mwa Somalia.
Kwa mujibu na taarifa iliyotolewa na serikali, wanajeshi wa Kenya walitwaa bundiki 11 aina ya AK-47, vifaa vya mawasiliano, chakula na sare za kijeshi.
Uvamizi huo wa siku ya Jumapili ulifanya na vikosi vya nchi kavu vikisaidiwa na helkopta za jeshi.
Serikali ilichapisha picha za badhi ya silaha jeshi lilitwaa ikiwemo milipuko ya kujitengenezea.

Baadhi ya vilupuzi vilivyotwaliwa kutoka kwa al-shabab

Kenya kwanza ilipeleka wanajeshi nchini Somalia mwezi Oktoba mwaka 2011 katika kile kilichojulikana kama Oparesheni Linda Nchi, kabla ya kujiunga na kikosi cha Muungano wa Afrika kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa nchini Somalia mwaka uliofuatia.
"Tulisikia sauti za ndege zikishambulia sehemu ya Badhade, lakini hatujui hasara iliyotokana na shambulio hilo. Sijui ni kitu gani wanajeshi wa Kenya wanatuhumu kuona katika eneo hilo na hali hawakutujulisha chochote kuhusiana na mashambulizi hayo." alisema mkuu wa wilaya ya Badhade Farah Heibe.
"Igekuwa bora kama wangefahamisha jeshi la Somalia na wakuu wa utawala kuhusu shambulio hilo. Siyo jambo la busara kushambulia maeneo yetu bila ya kuwasiliana nasi, kama nchi huru."

0 comments:

Post a Comment