Social

Monday, March 27, 2017

JPM apokea ripoti ya CAG


Dar es Salaam. Rais John Pombe Magufuli amepokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu leo, imeeleza kuwa  ripoti hiyo imewasilishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa  Mussa Assad.
Ripoti hiyo imegusa maeneo mbalimbali yakiwamo ukaguzi wa hali ya hesabu za Serikali, misamaha ya kodi, ukusanyaji wa kodi na maduhuli ya Serikali, uandaaji na utekelezaji wa bajeti, hali ya deni la Taifa, usimamizi wa rasilimali watu, usimamizi wa mali na madeni ya Serikali na usimamizi na uendeshaji wa taasisi za umma zikiwemo taasisi muhimu za kifedha na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

0 comments:

Post a Comment