Social

Friday, March 31, 2017

Mourinho asalimu amri kwa Neymar



Barcelona. Mpango wa Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho kumsajili nyota wa Barcelona, Neymar JR umefutwa kutokana na ugumu wa kumng'oa.
Mourinho alisema anaamini nyota huyo wa Barcelona haiwezekani kuondoka katika kikosi chake kwa sasa.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil kwa nyakati tofauti amekuwa akihusisha kujiunga na miamba hiyo ya Old Traford, huku ikiripotiwa wiki hii kwamba klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England iliahidi kuvunja benki ili kuinasa saini ya nyota huyo.
Hata hivyo, Kocha Mourinho amefuta mpango huo na kusema kumsajili Neymar ni jambo gumu na lisilowezekana kwa sasa.
"Ninapenda kuwa mkweli kwa klabu yangu na kuwaelezea yale ambayo wamenituma kuyafanya," amesema Mourinho alipozungumza na gazeti la ESPN Brazil.
Amesema, "Neymar ni mchezaji tegemeo. Klabu kama Barcelona haiwezi kukubali kumwachia aondoke. Japokuwa naye Messi ambaye ni mchezaji kijana na tegemeo kwa baadaye pia amekuwa akicheza kwa kiwango cha juu licha ya kufikisha miaka 30."
Aliongeza kuwa, "Neymar atakuwa mchezaji mahiri katika kikosi cha Barcelona akimfuatia Messi. Nafikiri kumsajili ni sawa na kumtoa kwenye usalama. Siyo jambo rahisi kumsajili."
Neymar (25) amefunga mabao 14 katika mashindano yote msimu huu ikiwa ni mabao machache tangu alipojiunga na klabu hiyo msimu wa 2013-14.

0 comments:

Post a Comment