Iinga. Bundi ametua Lipuli FC iliyopanda Ligi Kuu mwaka huu baada ya kuongozi wake kugawanyika makundi mawili.
Tangu kupanda kwa timu hiyo viongozi wa klabu hiyo wamekuwa katika mgogoro kati ya mwenyekiti na katibu wake.
Kundi la kwanza katika timu hiyo linaoongozwa na Katibu Mkuu wa Lipuli, Willy Chikweo akiongozwa na kaimu mwenyekiti wa timu hiyo Davotta Chaula.
Huku kundi la pili likiwa chini ya mwenyekiti wa timu hiyo aliyekuwa amefungiwa na Chama cha Soka Mkoa wa Iringa (IRFA), Abuu Changawa (Majeki).
Mzozo huo ulianza Juni mwaka jana wakati IRFA ilipomfungia Changawa kwa kipindi cha miezi 12 kutojihusisha na masuala ya soka kwa madai ya kukiuka maadili ya mchezo huo kwa viongozi wa chama hicho.
Hata hivyo, baada ya Lipuli kupanda daraja uongozi wa IRFA uliamua kumsamehe Changawa na kumtaka kuendelea na majukumu yake ya uongozi ndani ya timu. Baada ya kufunguliwa Changawa, Kamati tendaji ya Lipuli iliyoketi chini ya makamu mwenyekiti Chaula na katibu mkuu Chikweo na wajumbe wengine ilitangaza kumsimamisha uanachama kwa madai kuwa haijaridhishwa na mwenedo wake wakati alipokuwa akitumia adhabu yake ya kufungiwa.
Akizungumza suala hilo Katibu Msaidizi, Lonjino Malambo alisema mwenyekiti wao alikiuka taratibu za adhabu mara baada ya kufungiwa kwani alijihusisha na masuala ya michezo ikwia kuratibu Kombe la Msofa.
"Kipindi chote alichokuwa amepewa adhabu na IRFA sisi kamati tendaji tulikuwa tunafuatilia nyendo zake, na ndipo tulipoona yapo maeneo mengi amekiuka na kwa mujibu wa katiba hii tumeamua kumfungia kwa muda miezi 12 asijihusisha na Lipuli FC," alisema Malambo.
Akijibu madai hayo Changawa 'Majeki' alisema hatambua adhabu hiyo kwa kuwa kamati iliyoketi kumjadili wajumbe wake hawana sifa za kuwapo kwenye kikao hicho. "Mimi ninasimamia Katiba ya Lipuli FC, niseme kweli hata hawa waliokaa vikao na kutoa adhabu kwangu hawana mamlaka hayo, mimi ni mwenyekiti na ninatekeleza makujumu yangu kwa kusimamia katika…ninaona vikao walivyokaa ni sawa na vikao vya harusi"alisema Changawa.
"Timu hii siyo ya kikundi fulani …nitahakikisha ninaicha katika mikono salama, wananchi wa Iringa wasiwe na wasiwasi kuanzia sasa wajitokeza kuchukua fomu za kujiunga kuwa wanachama wa timu kwani hatua hiyo itasaidia kupata fedha, pia kupata viongozi bora wa kuiongoza Lipuli FC" alisema.
Shabiki wa Lipuli, Rafel Mtitu aliwataka viongozi hao kukaa meza moja kumaliza tofauti zao ili kupanga mipango bora ya timu kushiriki Ligi Kuu.

0 comments:
Post a Comment