Bukoba. Hatua ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kuwakatia huduma hiyo wateja wake wanaodaiwa imeanza kuwaathiri wananchi.
Taasisi na idara mbalimbali zinazotumia maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Bukoba (Busawa) ndizo zilizoathirika zaidi baada ya mamlaka hiyo inayodaiwa Sh500 milioni kukatiwa umeme.
Mtaalamu wa ufundi wa Buwasa, Charles Chibuga alisema deni hilo linapaswa kulipwa na Wizara ya Maji kwa mujibu wa makubaliano ya uendeshaji wa mradi huo.
Kaimu Meneja wa Tanesco Mkoa wa Kagera, Mhandisi Felix Olang alisema wanatekeleza agizo la Rais John Magufuli la kuwakatia umeme wadaiwa sugu. Alisema taasisi nyingine zilizokatiwa umeme ni Polisi inayodaiwa Sh30 milioni na Magereza (Sh60 milioni).
0 comments:
Post a Comment