Biharamulo. Mkuu
wa Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera, Saada Malunde amesema kuanzishwa kwa
tovuti za kila halmashauri kote nchini kutasaidia kupatikana kwa maendeleo ya
haraka katika nyanja mbalimbali.
Malunde
alitoa kauli hiyo juzi wakati akizindua tovuti ya halmashauri hiyo itakayokuwa
ikitumika kufahamisha jamii mambo mbalimbali yanayofanywa kwa ajili ya
maendeleo ya wilaya.
Ofisa
habari wa halmashauri hiyo, Jonathan Xavery alisema tayari wameshatoa mafunzo
kwa maofisa habari na wachambuzi wa mifumo ya kompyuta 35 kutoka mikoa
ya kanda ya ziwa ambayo ni Kagera, Mara , Mwanza, Shinyanga na Simiyu.
“Tovuti
yetu itajulikana kwa jina la www.biharamulodc.go.tz na kila kitu kitakuwa
kikionekana kila kinapofanyika kwa wale watakaofungua muda wa tukio,”alisema
0 comments:
Post a Comment