Social

Thursday, April 13, 2017

Wazabuni wampelekea madeni Rais JPM


Tanga.Wazabuni  wanaotoa huduma katika taasisi mbalimbali Mkoani Tanga,wameamua kumuomba Rais John Magufuli kuingilia kati ili walipwe madeni yao wanayodai  kwa muda mrefu.
Wamesema wameamua kumuomba Rais kuingilia kati baada ya kugonga mwamba kwenye ngazi nyingine ambako wamekuwa wakipewa ahadi zilizotekelezeka huku wakiidai Serikali zaidi  ya Sh 3bilioni.
Walitoa ombi hilo walipozungumza na waandishi wa habari leo jijini hapa kuhusiana na ukata uliowakumba kutokana na fedha zao kuwa Serikalini.
Wazabuni hao wamesema kuwa madeni hayo yamaesababisha baadhi yao kusitisha huduma katika baadhi ya taasisi kutoka na kushindwa kumudu gharama za uendeshaji.
Mwenyekiti Umoja wa wazabuni hao Bashiri Kajembe alisema kuwa malimbikizo hayo ya madeni ni toka kuanzia mwaka 2013 hadi 2016 ambao serikali imeshindwa kuwalipa kwa wakati.

0 comments:

Post a Comment