Dar es Salaam. Bima Mpya ya afya iliyozinduliwa leo jijini hapa imejipanga kuwapa huduma bora na yenye gharama nafuu watu wenye kipato cha chini.
Akizungumzia wakazi wa uzinduzi wa bima hiyo leo Alhamisi, Ofisa Mtendaji wa Wakala la Bima Zurich Simba alisema huduma hiyo itatolewa kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya Jubilee.
"Bima hii mpya inaitwa Afya Wote inachangiwa shilingi 174,000 kwa mwaka inahusu familia ya watu wanne yaani baba, mama na watoto wawili, inakuwa na thamani ya Sh2,500,000 kwa mwaka, tayari imetambuliwa na Serikali na inatumika kwenye hospitali kubwa ikiwamo ya Taifa ya Muhimbili,"alisema
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Temekem Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya Edward Mbaga alisema Serikali inafurahi kuona huduma ya Bima ya Afya inazidi kustawi na hivyo kuwanufaisha wananchi wa vipato vya viwango tofauti.
0 comments:
Post a Comment