London, England.UONGOZI wa Arsenal umeibuka na kumtamkia Alexis Sanchez; "Saini mkataba mpya au uhamie PSG." Imefahamika kuwa kocha Arsene Wenger bado anamhitaji mchezaji huyo lakini kuna habari kwamba mchezaji huyo ni lazima ataondoka.
Kocha huyo anafahamu kwamba klabu za Chelsea na Manchester City zinataka kumsajili mchezaji huyo lakini hawapo tayari kumtoa kwenda kwa wapinzani wao na balada yake wanataka kumuuza kwa PSG.
Wenger ni rafiki wa Rais wa PSG Nasser Al- Khelaifi na kuna habari kwamba mazungumzo ya awali yameshafanyika.
0 comments:
Post a Comment