Yande Media Unaonaje soko la Fasheni Tanzania
Felisiani: Fashion Tanzania n ngumu, kazi zipo chache na mara nyingi hazitangazwi mtu anatafuta model wake kimya kimya so wenye majina ndo wanapata, na jamii bado haiipi kipaumbele kikubwa kuwawezesha wasanii kupata maisha mazuri
Yande Media: Umejipangaje kuweza kutoboa kwenye hili soko gumu
Felisiani: Nina hakikisha network yangu inakua, natengenezwa mwili wangu ili uwe wa kimataifa, sasa nipo natengeneza branding yangu na najiandaa kuja dar kutafuta kazi maana huku Tanga ni chache sana
Yande Media: Nini Changamoto kubwa sana zinazokurudisha nyuma
Felisiani: Fani yetu inahotaji mavazi mengi, kwa hali liyopo inakuwa ngumu kupata ladha tofauti ya mwonekano ila akipatikana mbunifu atasaidia sana kunipa mwonekano mzuri
Felisiani: Ugumu wa kupata management katika kazi inashusha mori kabisa ila napambana najua nitafanikiwa kupata soon
Felisiani: Dar es Salaam kuna professional Photographers wengi ila huku ni wa chache hivyo kufanya wawe na bei kubwa na kwa model mpya hiyo ni Changamoto
Yande Media: Unazungumziaje hali ya sanaa nchini na hali ya kutekwa wasanii na kukamatwa kila kukicha
Felisiani: Muda ndo tiba ya kila ugonjwa, mambo haya ni magumu hasa hili la akina Roma liliniumiza moyo klichobaki ni kumlilia Mola maana yeye ndio aliyeweka serikali na ndiyo mtoa riziki
Mawasiliano ya Felisiani
071707196
0 comments:
Post a Comment