Social

Friday, April 28, 2017

Ulinzi waimarishwa Udom, JPM akisubiriwa


Dodoma. Rais John Magufuli leo anatarajia kuzungumza na wanajumuiya wa Chuo Kikuu cha Dodoma(Udom).
Ulinzi umeimarishwa katika ukumbi wa Chimwaga, udoma  huku maofisa usalama wakifunga mashine za kukagulia magari katika barabara za kuingilia chuoni hapo.
Kadhalika,  waliokuwa wakiingia katika ukumbi huo waliamriwa kuzima simu zao hadi pale watakapotoka ndani ya ukumbi huo.
Pamoja na hilo, leo Rais atakabidhiwa orodha ya watumishi kwenye vyeti feki katika mkusanyiko huo sambamba na kusherekea miaka 10 tangu kuanzishwa chuo hicho ambacho kilianzia katika ukumbi wa Chimwaga zamani  ukimilikiwa na CCM.

0 comments:

Post a Comment