Social

Thursday, April 27, 2017

Mahakama yampa Ole Nangole siku 14




Arusha .Mahakama kuu kanda ya Arusha imempa siku 14 aliyekuwa mbunge wa Longido Onesmo Ole Nangole kuleta notisi ya kukata rufaa nje ya muda.
Akitoa uamuzi huo ,Jaji Sekela Moshi amesema mahakama imeamua kumuongezea muda mara baada ya muombaji huyo wa kwanza ambaye ni Onesmo Nangole kuiomba mahakama imuongezee muda kutokana na ukiukwaji wa sheria wakati alipokuwa anaanda notisi hiyo.
 Awali, mahakama ilimvua ubunge Ole Nangole na kuamuru uchaguzi urudiwe upya.

0 comments:

Post a Comment