Tabora.Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry amesema wanahabari wanatakiwa kubeba dhamana kuhakikisha Taifa haliathiriwi na matumizi ya dawa, vipodozi, vyakula au vifaatiba visivyokidhi viwango ili kulinda afya za wananchi.
Mwanry amesema hayo leo kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora alipokuwa akifungua kikao kazi cha kuhamasisha usimamizi wa Sheria ya Chakula, Dawa, Vipodozi, Sura 219 kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini.
"Mkiwa wadau muhimu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TDFA), mnao mchango mkubwa katika kuifikia jamii na kuifanya ibadili mitizamo mbalimbali iliyopo kuhusiana na mazoea ya matumizi ya bidhaa zisizofaa na zenye madhara kwa wananchi hususan vipodozi vyenye viambato dumu vilivyopigwa marufuku," amesema.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TDFA, Hiiti Sillo amesema taasisi yake imekuwa ikitoa elimu kwa wadau mbalimbali ili kuongeza wigo wa ufahamu wa shughuli zake na kuzitumia katika kulinda afya ya jamii.
0 comments:
Post a Comment