Social

Friday, April 28, 2017

Walioghushi vyeti kutupwa jela miaka saba, JPM akabidhiwa ripoti


Dodoma. Waziri wa Utumishi, Angela Kairuki amemkabidhi Rais John Magufuli  majina ya watumishi wenye vyeti feki huku akieleza kuwa waliobainika kughushi vyeti watahukumiwa kifungo cha miaka saba jela kulingana na kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2016.
Kairuki amesema sheria hizo pia zinawaweka hatiani mawakala wote wanaotumika kutengeneza vyeti feki.
Amesema kanuni za utumishi wa umma za 2016, zinaeleza kuwa muombaji wa nafasi za ajira serikali ni akitoa taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kijinai na kinidhamu.

0 comments:

Post a Comment