Mawazo mengine! Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho katoa
mpya, jana Jumapili timu yake ilikuwa inacheza na Southampton mechi ya fainali
ya Kombe la Ligi, lakini mawazo yake hayapo.
Hakuwa akiiwazia mechi hiyo na wala
hakuwa akimuwazia Wayne Rooney na sakata lake, akili na mawazo yake ni mechi ya
robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Chelsea itakayopigwa Machi 13.
Kocha huyo ameanza mchecheto na kusema
ana wasiwasi na matokeo kwa kuwa ana msongamano wa mechi kabla ya mchezo huo na
ratiba inaweza kuchangia timu yake ifanye vibaya.
Ushindi wake wa mabao 2-1 dhidi ya
Blackburn haufikirii sana, lakini akasema kichwa chake kimejawa na ratiba ngumu
kabla ya kuibukia kwa mpambano huo wa Stamford Bridge.
“Sina cha kujibu,” alisema. “Nimeanza
mechi na St Etienne Jumatano, mechi ya Kombe la Ligi Jumapili (jana) halafu
wanakuja Bournemouth Machi 4 kisha mechi ya Europa Raundi ya 16 dhidi ya FC
Rostov Machi 9 halafu Chelsea Machi 13.”
Ninalazimika kucheza tu ikiwemo mechi
hiyo ya Ulaya. Na papo hapo kucheza kuwania nafasi ya nne Ligi Kuu England.
“Chelsea wanalitaka Kombe la FA najua
watakomaa tu, kwa kuwa wanataka ubingwa na sisi lazima tupambane.”
Alisema anajua Antonio Conte anataka
kumuonyesha Mourinho ambaye timu yake ndiyo bingwa mwaka huu, kocha wa Chelsea
anaitazama mechi ya United kwa kujiamini. “Kwanza hana presha ya mchezo na
matokeo ya mwisho, Oktoba mwaka jana Chelsea iliifunga Man United 4-0 mechi
iliyopigwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.”
Matokeo hayo yalimuumiza Mourinho kwani
kilikuwa kipigo cha mwaka katika historia ya ligi kuu kwake.
Man United imekuwa ikisumbuka kwa
Chelsea kwani ilishinda mara mbili Stamford Bridge miaka 15 iliyopita.
Mourinho aliwapongeza wachezaji wake
kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya St Etienne katika Ligi ya Europa na akawataka
kukomaa licha ya kuwa na ratiba ngumu.
0 comments:
Post a Comment