Mtu mwengine aliyeteuliwa na rais wa Marekani Donald Trump, kujaza wadhfa
wa waziri wa jeshi la wanamaji amejiondoa baada ya kuonekana kukiuka sheria za
taifa kuhusu mgongano wa maslahi.
Philip Bilden ameeleza
wasiwasi wake kuhusu maisha yake ya usiri na changamoto alizokumbana nazo
katika kujitenganisha na biashara zake.
Waziri wa usalama, Jim
Mattis, amesema atampendekeza mtu atakayechukua nafasi ya Bilden katika kipindi
cha siku chache zijazo.
Mteuliwa wa Rais Trump
aliyependekezwa kusimamia jeshi la Marekani alijiondoa mapema mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment