Dar es Salaam. Kama ni ushindi wa awali, basi unaweza kusema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye juzi nusura alale mahabusu polisi alikoitwa kwa mahojiano ya tuhuma za dawa za kulevya, amepata baada ya Mahakama Kuu kumpa kinga ya muda inayozuia kumkamata na kumweka kizuizini.
Mbowe aligoma kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam tangu alipotakiwa kufanya hivyo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliyetaka watu 65 akiwamo mwanasiasa huyo waripoti Februari 10.
Juzi, Mbowe alikamatwa na kuachiwa usiku mwingi na jana akaibuka Mahakama Kuu, ambako amefungua kesi ya kikatiba, ambayo pamoja na mambo mengine, anapinga mamlaka ya wakuu wa mikoa kukamata na kile anachokiita kudhalilisha watu.
Uamuzi huo ulitolewa jana na jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu; Sekieti Kihiyo, Lugano Mwandambo na Pellagia Kaday kutokana na kesi aliyoifungua Mbowe, Februari 10.
Mbowe alifikia hatua hiyo baada ya Makonda kumtaja katika orodha ya watu 65 aliowataka waripoti polisi kwa mahojiano kuhusu matumizi na biashara ya dawa za kulevya.
0 comments:
Post a Comment