Social

Monday, March 6, 2017

Wazabuni kwenda kwa Majaliwa kudai Sh5 bilioni




Mbeya. Wazabuni  wanaotoa huduma kwenye taasisi za umma mkoani hapa wamepanga kwenda Dodoma kumuona Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa awasaidie walipwe madeni yao yanayofikia zaidi ya Sh5 bilioni.
Mwenyekiti wa Chama cha Wazabuni mkoani hapa (Chawambe), Mustafa Ngonyani  amesema wanadai fedha hizo tangu mwaka 2011 baada ya kutoa huduma kwenye taasisi za umma hususan hospitali, vyuo vya uuguzi, shule na magereza.
Ametaja baadhi ya taasisi zilizopata huduma  kupitia wazabuni hao kuwa ni Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya, magereza yote mkoani hapa, Chuo cha Kilimo Uyole, Igurusi, vyuo vya uuguzi, Tukuyu, Mbeya na shule mbalimbali za msingi na sekondari.
Ngonyaji amesema walishafikisha hoja zao Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na taasisi zinazodaiwa  lakini hakuna walichosaidiwa zaidi ya kupewa maneno ya kukatisha tamaa.

0 comments:

Post a Comment