Social

Wednesday, June 21, 2017

Lewandowski amuwashia moto kocha Ancelotti kwa kumkosesha kiatu cha dhahabu Bayern Munich



Munich, Ujerumani. Wakala Maik Barthel anayemsimamia mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert Lewandowski, amesema mchezaji huyo amevunjika moyo kutokana na kukosa ushirikiano kutoka uongozi wa juu ili aweze kumaliza mfungaji bora.
Mchezaji huyo raia wa Poland alimaliza msimu ulioisha akiwa amefikisha mabao 30 ikiwa ni nyuma ya bao moja dhidi ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang aliyenyakua kiatu cha dhahabu akiwa amefikisha mabao 31.
Hivyo mchezaji huyo kupitia kwa wakala wake, ameutupia lawama uongozi wa klabu hiyo kwa kutompa ushirikiano hasa kocha wake Carlo Ancelotti.
Aubameyang alimzidi mwenzake baada ya kufunga bao katika mchezo wao wa mwisho wa Bundersliga walipoilaza Werde Bremen mabao 4-3, huku Lewandowski akishindwa kufunga bao mchezo wao wa mwsho dhdi ya Freiburg walipoibuka 4-1.
Hivyo mchezaji huyo ameutupia lawama uongozi wa klabu hiyo kwa kutompa ushirikiano hasa kocha wake Carlo Ancelotti.

0 comments:

Post a Comment