Dar es Salaam. Mwanasheria nguli wa Kenya, Profesa Patrick Lumumba amesema mkwamo wa maendeleo uliopo katika nchi za Afrika unasababishwa na siasa chafu miongoni mwa viongozi wa mataifa ya Afrika.
Lumumba ameyasema hayo leo Alhamisi, katika Kongamano la Kigoda cha Mwalimu Nyerere kinachoendelea kwa siku ya tatu jijini hapa.
Profesa Lumumba amesema Waafrika wanapaswa kujiamini na kushikamana sanjari na kutakatisha siasa za nchi zote.
"Nchi zetu haziwezi kuendelea kwa bajeti zinazotegemea wahisani ni lazima kuvipenda vitu vyetu na kuvithamini," amesema Lumumba katika kongamano hilo.
Ukumbi wa Nkrumah katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lilipofanyika kongamano hilo kwa siku tatu, ulifurika mamia ya watu.
Kabla Profesa Lumumba hajaanza kuzungumza, wasifu wake ulisomwa kwa zaidi ya dakika tatu na msomaji alisema hakuweza kuumaliza.
0 comments:
Post a Comment