Social

Friday, June 16, 2017

Benki ya Dunia yazindua shindano la Blog4Dev


Dar es Salaam. Benki ya Dunia (WB) imezindua shindano la kuandika katika mtandao wa kijamii aina ya blogu, liitwalo, Blog4Dev.
Shindano hilo lililozinduliwa leo (Alhamisi) litawahusisha vijana wa kitanzania wenye umri wa kati ya miaka 18 na 28 wanaoishi nchini katika nchi za Tanzania, Malawi, Somalia na Burundi.
"Wanaweza watakwenda jiji la Washington D.C, Marekani, yalipo makau makuu ya Benki hii, Oktoba mwaka huu," amesema , Bella Bird ambaye ni Mkurugenzi wa WB kwa nchi za Tanzania, Malawi, Somalia na Burundi.
Ameongeza; "Tumehamasika kuongeza ushindani na kujumuisha nchi nyingi zaidi kwa sababu tumeona ni njia bora zaidi ya kusaidia kupata vijana wa kike na kiume katika nchi hizo watakaojihusisha kikamilifu na masuala ya maendeleo katika nchi zao wakati wakijaribu kushinda tuzo ya shindano hili."
 Taarifa ya WB imesema washindi wawili kutoka Tanzania wataungana na wenzao kutoka Malawi, Somalia na Burundi jijini Washington D.C. yalipo makao makuu ya Benki ya Dunia.
Kadhalika, washindi wengine wawili watateuliwa kufanya kazi kwa wiki mbili katika ofisi za Benki ya Dunia kwenye nchi zao ambako watajifunza zaidi shughuli zinazofadhiliwa na Benki katika nchi zao na kuhusu michakato ya kubuni na kutekeleza miradi.

0 comments:

Post a Comment