Social

Thursday, June 15, 2017

Manusura wa ajali ya Lucky Vincent watolewa vyuma mwilini


Sioux. Watoto wawili  manusura wa ajali ya basi la Shule ya Msingi ya Lucky Vincent, Saidia Ismail na Wilson Tarimo wameondolewa vyuma walivyowekewa mwilini na kuanzia sasa wataweza kuoga wenyewe bila msaada wa wauguzi au wazazi.
Watoto hao walipata ajali  ya basi Mei 6 mwaka huu wakati wakienda katika mitihani ya ujirani mwema, ambapo wanafunzi wenzao 32, walimu wawili na dereva walifariki dunia.
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameandika katika ukurasa wake wa facebook leo Alhamisi na kueleza maendeleo ya watoto hao.
Manusura mwingie, Doreen Mshana, yeye alitolewa baadhi ya vyuma jana.
Walipelekwa kwenye kituo cha mishipa ya fahamu na uti wa mgongo, huko Dakota Dunes, ambako kazi hiyo ilifanyika jana. Tuendelee kuwaombea," amesema Nyalandu.

0 comments:

Post a Comment