Kwa ufupi
Washtakiwa hao wanadaiwa kuongoza, kupanga uhalifu na kukutwa na shehena ya samaki ambazo hazijalipiwa kodi zikiwa zimefungwa kwenye maboksi 2,579 kila boksi likiwa na uzito wa kilo 10 na zina thamani ya Sh 206 milioni.
By Godfrey Kahango, Mwananchi
Mbeya. Watu saba wakiwamo, wafanyabiashara wa samaki jijini Mbeya, maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa Tunduma na madereva wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkazi Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za uhujumu uchumi.
Washtakiwa hao wanadaiwa kuongoza, kupanga uhalifu na kukutwa na shehena ya samaki ambazo hazijalipiwa kodi zikiwa zimefungwa kwenye maboksi 2,579 kila boksi likiwa na uzito wa kilo 10 na zina thamani ya Sh 206 milioni.
Washtakiwa hao ni wafanyabiashara wa samaki jijini hapa, Joseph Mushi, Said Ramadhani, wakala wa mpakani mwa Tanzania na Zambia upande wa Tunduma Agripa Benjamini, Ofisa wa TRA-Tunduma, Andrew Ngachengo. Wengine ni Shaban Sankwa, Said Sisige na Pius Joseph wote wakiwa ni madereva wa gari lililokutwa na shenena ya samaki.
Mawakili wa Serikali, Basilusi Namkambe na Ahmed Stambuli wamedai mahakamani hapo kwamba washtakiwa kwa pamoja, kati ya Desemba 22, 2016 na Januari 22 mwaka huu walipanga uhalifu na kukutwa bidhaa ambazo hazijalipiwa kodi jijini hapa wakitokea China.
0 comments:
Post a Comment