Social

Monday, February 13, 2017

Steinmeier achaguliwa Rais mpya wa Ujerumani


Waziri wa zamani wa mashauri ya nchi za nje wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, amechaguliwa kuwa rais mpya ya Ujerumani, pale wabunge na waakilishi wa taifa walipopiga kura hii leo.
Bwana Steinmeier anaungwa mkono na vyama vikuu vya kisiasa.
Mwaka jana, alipokuwa waziri wa mashauri ya nchi za nje, alimuelezea Donald Trump kuwa mhubiri wa chuki
Baada ya uchaguzi wa Marekani, alisema, anapata shida kutambua msimamo wa Bwana Trump kuhusu sera zake za mashauri ya nchi za nje.
Rais wa Ujerumani hana madaraka ya utendaji, lakini anafikiriwa kuwa kiongozi wa maadili ya nchi.


Wabunge wa UjerumaniHaki miliki ya picha
Image capti

0 comments:

Post a Comment