Social

Monday, February 13, 2017

Lilipoonekana Gari la Manji baada ya kuchukuliwa na Ambulance Polisi


Source Millard Ayo
Jana jioni February 12 2017 Mfanyabiashara maarufu Yusuph Manji kwenye kituo cha Polisi Kati Dar es salaam alionekana akichukuliwa na gari la Wagonjwa aina ya Land Cruiser ikiwa ni baada ya kuhojiwa na Polisi toka Alhamisi February 9.
Baada ya gari hilo kumchukua haikujulikana alikopelekwa lakini halikuondoka peke yake kituoni hapo, gari lililoongoza msafara huo lilikua gari aina ya Range Rover linalomilikiwa na Mwenyekiti huyo wa Yanga.
Taarifa ilizopata millardayo.com na AyoTV ni kwamba msafara huo ulikwenda moja kwa moja kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Muhimbili Dar es salaam ambako watu mbalimbali wanaosumbuliwa na moyo hupata matibabu.
Hii picha hapa chini ni gari hilo aina ya Range Rover likiwa nje ya Taasisi hiyo ya moyo ambapo millardayo.com na AyoTV zinaendelea kufatilia zaidi kujua kinachoendelea.

0 comments:

Post a Comment