Dodoma. Miaka sita iliyopita, Bunge liligawanyika wakati rais wa wakati
huo, Jakaya Kikwete alipoingia bungeni kutoa hotuba ya kulizindua;
wapinzani walisimama na kutoka nje, CCM wakabaki wakiwazomea.
Jana ilikuwa tofauti; wabunge wa vyama vyote walipiga kelele kushangilia
mara alipotangazwa kuwa angeingia ukumbi wa Bunge na kelele zikawa maradufu
alipotambulishwa, na wote walikuwa na sababu za shangwe hizo.
"Kushangilia kulikuwa na lengo la kuionyesha jamii kuwa kiwango cha uongozi
cha Kikwete kilikuwa ni juu.," alisema mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji
Peter Msigwa baada ya kutoka ukumbini.
Kikwete, ambaye aliongoza Serikali ya Awamu ya Nne, alitinga bungeni
kumsindikiza mkewe, Salma ambaye jana alikuwa anaapishwa baada ya kuteuliwa
na Rais John Magufuli kuwa mbunge.
Tofauti na miaka ya nyuma wakati alipokuwa akiingia kwenye ukumbi huo akiwa
mbunge, waziri na baadaye Rais, Kikwete jana alikaa sehemu ya wageni, na
hata juhudi za kutaka Bunge livunje kanuni ili aingie sehemu wanayokaa
watunga sheria, hazikufanikiwa.
Kikwete, aliyeongozana na mtoto wake anayeitwa Ally, aliwasili ndani ya
ukumbi wa Bunge saa 2:55 asubuhi.
Tofauti na siku nyingine ambazo Spika Job Ndugai hutambulisha wageni baada
ya kipindi cha maswali na majibu, jana alibadili utaratibu kwa
kumtambulisha Rais Kikwete kabla ya kipindi cha maswali na majibu mara
baada ya Mama Salma kuapishwa.
"Nilikuwa nasubiri kidogo nione Mama (Salma Kikwete) anakaa wapi. Naomba
nichukue fursa hii kuwatambulisha wageni maalumu walio katika gallery ya
Spika," alisema Spika Ndugai mara baada ya kuapishwa kwa Mama Salma.
"Na mgeni wetu wa siku ya leo, si mwingine bali ni Rais mstaafu, Mheshimiwa
Jakaya Kikwete."
Kabla hajamaliza wabunge wote walianza kupiga makofi, vigelegele na kelele
za shangwe zilizodumu kwa takriban dakika tatu.
Akiwa eneo hilo la wageni, Rais Kikwete alisimama na kuinamisha kichwa
kuonyesha kushukuru, lakini kelele hizo ziliendelea na kumlazimisha
kiongozi huyo kunyoosha mikono tena kuwashukuru.
"Kwa makofi hayo, sasa naomba mumpe standing ovation (kumuonyesha heshima
kwa kusimama," alisema Spika Ndugai.
Ndipo wabunge waliposimama na kuendelea kupiga meza kwa nguvu kushangilia,
huku Kikwete akinyoosha tena mkono kuwashukuru.
"Tunakumiss, tunakumiss," zilisikika sauti za baadhi wa wabunge waliofungua
vipaza sauti vyao kunogesha shangwe hizo.
Baadaye, Spika Ndugai alieleza yake ya moyoni.
"Waheshimiwa wabunge, binafsi mimi ni kipindi cha nne (bungeni), sijawahi
kuona mgeni amepokewa kwa kiwango hiki," alisema Spika.
Aliposema hayo, wabunge walilipuka tena kwa shangwe.
Licha ya kuwasihi wabunge hao na kuwataka watulie, waliendelea kushangilia
huku baadhi wakitaka watengue kanuni ili Rais Kikwete aingie ndani ya Bunge
na kusalimiana na Spika.
"Kwa kushangilia huko inaonyesha kuwa hata waliommiss wapo," alisema Ndugai.
Alipoulizwa nje ya ukumbi kuhusu mwongozo aliotaka kuomba, Mbunge wa Kigoma
Mjini, Zitto Kabwe alisema alitaka Spika amruhusu Kikwete aingie ndani ya
ukumbi wa Bunge.
Hata hivyo, Ndugai hakulikubali jambo hilo na badala yake Bunge liliendelea
na ratiba yake ya maswali na majibu.
Kikwete, aliyekaa ndani ya ukumbi wa Bunge kwa takribani dakika 30,
aliondoka baada ya utambulisho huo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti bungeni jana, wabunge wa upinzani walisema
walimshangilia Rais Kikwete kwa sababu aliruhusu kukosolewa, kushauriwa na
alikubali kuchukua ushauri wa watu tofauti.
"Tulimshangilia kwa sababu aliruhusu demokrasia," alisema Mchungaji Msigwa.
"Kikwete alivumilia vitendo vya kutoka bungeni kwa sababu alifahamu kuwa
hiyo ni demokrasia ambayo inafanyika kote duniani kama njia ya kuonyesha
watu hawakubaliani na jambo fulani. Lakini hivi sasa tukifanya hivy
0 comments:
Post a Comment