Kwa ufupi
Rais huyo
wa Kenya, Uhuru Kenyatta alirekodi video hiyo Jumatano akiwa na kundi hilo na
anaonekana akijaribu kudansi sambamba na madansa hao wakati wakicheza wimbo wa
“Bamba Kura Yako” unaohamasisha vijana kujiandikisha kupiga kura.
By Mwandishi Wetu, Mwananchi
Dar es
Salaam. Rais amezua kizaazaa baada ya kurekodi video akicheza muziki na kundi
la madansa la FBI akiwa Ikulu ya Nairobi, jambo lililosababisha wananchi
wamshambulie kwenye mitandao ya kijamii.
Rais huyo
wa Kenya, Uhuru Kenyatta alirekodi video hiyo Jumatano akiwa na kundi hilo na
anaonekana akijaribu kudansi sambamba na madansa hao wakati wakicheza wimbo wa
“Bamba Kura Yako” unaohamasisha vijana kujiandikisha kupiga kura.
Kenyatta
anaonekana akiwa amevalia jaketi jekundu linalofanana na mavazi ya madansa hao,
lakini likitofautiana kwa rangi.
Madansa
hao wanaonekana wakiinamisha vichwa chini na kunyoosha mkono mmoja pembeni na
mwingine ukiwa umekunjwa sambamba na kichwa, mithili ya mtu anayelia akiwa
amejifunika uso.
Lakini
wananchi walihamaki kwenye mitandao ya kijamii wakimtaka aamke, wakitumia alama
(hash tag) ya #DabOfShame kumkosoa kutokana na kutotatua mgogoro na madaktari
ambao wamegoma tangu mwaka jana.
Madaktari
walianza mgomo Desemba 5 mwaka jana wakitaka ongezeko la asilimia 300 la
mishahara, kuangaliwa upya kwa mazingira ya kazi, mfumo wa kazi na vigezo vya
kupandishwa cheo, na utatuzi wa tatizo la upungufu wa wafanyakazi katika
hospitali za Serikali.
Mmoja wa
wachangiaji kwenye mitandao ya kijamiii aliyejitambulisha kwa jina la Juma,
aliliambia gazeti la Star kuwa Kenyatta anajishughuli zaidi kupiga danadana
madai ya madaktari.
Wauguzi wa
Kenya hawaelewi inakuwaje rais aweze kudansi wakati wagonjwa wakihangaika na
wengine kufariki.
“(Serikali)
Inawaambia wagonjwa waende kujiandikisha wakati hospitalia hazifanyi
kazi...nani amewaroga Wakenya,” alihoji Geoffrey Osiba akiongea na gazeti la
Star.
Wengine
walisema Kenyatta amechoka na hana budi kuruhusiwa kupumzika mwezi Agosti.
0 comments:
Post a Comment